Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi mepesi Nyamagana

23 Dec 2022 By simbasc 244 views
Kikosi chetu leo jioni kimefanya mazoezi mepesi ya utimamu wa mwili katika Uwanja wa Nyamagana baada ya kurejea kutoka mkoani Kagera. Kikosi kimefika jijini Mwanza jana jioni na wachezaji wakapewa mapumziko kabla ya kuanza mazoezi mepesi leo jioni. Moses Phiri ndiye mchezaji pekee ambaye hajashiriki mazoezi hayo baada ya kupata maumivu katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera. Kesho kikosi kitaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya KMC utakaopigwa Jumatatu katika Uwanja wa CCM Kirumba
Advertisement
Back to homepage
Share this story