Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi kujiandaa na Nusu Fainali

8 Jan 2022

Kikosi kimefanya mazoezi asubuhi katika Uwanja wa Mao Tse Tung kujiandaa na mchezo wa Nusu Fainali ya Michuano ya Mapinduzi utakaopigwa Jumatatu.

Mechi kati ya Azam FC na Namungo ambao wanamalizia mechi zao za makundi ndiyo itaamua timu ya kucheza nayo ambapo atakayemaliza nafasi ya pili ndiyo tutakutana naye nusu fainali.

Advertisement

Wachezaji wote wamefanya mazoezi na hakuna aliyepata majeruhi katika mchezo wetu wa jana dhidi ya Mlandege.

Wachezaji wameendelea kuonyesha uwezo mkubwa mazoezini ili kulivutia benchi la ufundi kwa ajili ya kutaka kupewa nafasi kwenye mchezo wa nusu fainali.

Back to homepage
Share this story