Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi jioni kujiandaa na KMC

22 Dec 2021

Kikosi chetu kimefanya mazoezi jioni katika Uwanja wa Shirika la Reli (TRC) mkoani hapa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa Ijumaa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Timu iliwasili saa tano asubuhi ambapo wachezaji walipumzika kwa saa nne kabla ya kuanza mazoezi ya kuweka miili sawa.

Advertisement

Wachezaji wote 24 waliosafiri wamefanya mazoezi na wapo kwenye hali nzuri hakuna aliyepata majeraha.

Aidha, kikosi kinatarajia kufanya mazoezi ya mwisho kesho kabla ya kushuka dimbani.

Back to homepage
Share this story