Simba Sports Club
News

Timu yaendelea na mazoezi Mo Arena

4 Mar 2023

Kikosi kimeingia kambini baada ya mazoezi ya jana jioni ya kujiandaa na mchezo huo ambao hatuitaji chochote zaidi ya ushindi.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi isipokuwa Kibu Denis ambaye amefanya peke yake chini ya uangalizi wa daktari kutokana na kupata maumivu katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Uganda.

Advertisement

Morali za wachezaji ipo juu na wanafanya jitihada kubwa mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi katika mchezo wa Jumanne.

Mchezo wetu dhidi ya Vipers utapigwa saa moja usiku katika dimba la Benjamin Mkapa na tayari vituo vimetangazwa ambapo tiketi zinapatikana.

Back to homepage
Share this story