Simba Sports Club
News

Timu yaendelea na Mazoezi Mo Arena

10 May 2023

Mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting utapigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Ijumaa saa moja usiku.

Timu ilianza mazoezi jana baada ya kurejea juzi kutoka mkoani Mtwara ilipocheza nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Azam FC.

Advertisement

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa kuipigania timu kuhakikisha tunapata pointi tatu siku ya Ijumaa.

Kwa sasa malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zetu tatu za ligi zilizosalia tukianza na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.

Back to homepage
Share this story