Simba Sports Club
News

Timu yaendelea na mazoezi Mo Arena

19 Oct 2022

Timu iliingia rasmi kambini jana kujiandaa na mchezo huo ambao unavuta hisia za mashabiki wengi ndani na nje ya nchi.

Wachezaji wote walioshiriki mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Premiero De Agosto mwishoni mwa juma lililopita wameingia kambini na wameshiriki mazoezi ya leo.

Advertisement

Morali ya wachezaji ipo juu na wanafanya kila linalowezekana kulishawishi benchi la ufundi lililopo chini ya Kocha Juma Mgunda ili kupata nafasi ya kucheza Jumapili.

Uongozi unahakikisha unalipa benchi la ufundi na wachezaji kila wanachohitaji ili kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo na kuwapa furaha Wanasimba.

Back to homepage
Share this story