Simba Sports Club
News

Timu yaendelea na mazoezi Mo Arena

2 Nov 2023 By simbasc 176 views
Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili, Novemba 5. Timu iliingia kambini Jumanne kujiandaa na mchezo huo mkubwa ambao unavuta hisia kali za mashabiki kote ndani na nje ya nchi. Wachezaji wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na morali yao iko juu lengo likiwa ni kuhakikisha tunapata alama tatu.
Advertisement
Back to homepage
Share this story