Simba Sports Club
News

Timu yaendelea kujifua Nchini Misri

25 Jul 2024

Kwa mujibu wa ratiba ya programu Leo kulikuwa na awamu mbili ambapo ilikuwa Gym huku wachezaji wakigawanyika kwenye makundi matatu tofauti na usiku walifanya wote kwa pamoja uwanjani.

Baada ya programu zote mbili za mazoezi kumalizika Kocha Mkuu, Fadlu amesema ilikuwa ratiba muhimu kwanza kuongeza utimamu wa mwili wa kila mchezaji na kuwa fiti zaidi ili kwenda kushindana kwenye kıla mechi bila ya kuonekana kuchoka kwa urahisi.

Advertisement

Fadlu amesema mazoezi ya mbinu yale ya jioni kuandaa wachezaji namna ya kucheza vizuri kwa kila mpinzani tutakayekutana nae, kuwa bora kwa ubora mkubwa.

“Kikubwa tunaendelea kufurahishwa na ushindani wa kila mchezaji ndani ya kikosi changu wanapambana kila mmoja kwa nafasi yake kuonyesha ubora aliokuwa nao,” amesema Kocha Fadlu.

Back to homepage
Share this story