Kikosi kimeingia rasmi kambini jana kujiandaa na mchezo huo ambao tunahitaji kupata matokeo mazuri ugenini ili mechi ya marudio nyumbani isiwe ya presha kwetu.
Wachezaji Pape Sakho ambaye alikuwa na matatizo ya kifamilia na Henock Inonga aliyepata maumivu kabla ya mchezo wetu dhidi Dodoma Jiji wapo vizuri na tayari wamejiunga na wenzao kuunda kambi hiyo.
Advertisement
Wachezaji wote wapo katika hali nzuri na morali ipo juu kuelekea mchezo huo ambapo kama tukifanikiwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote mbili tutaingia kwenye hatua ya makundi.