Kikosi kinatarajia kufika Dar es Salaam saa kumi alfajiri na moja kwa moja kitaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumatano ya wiki ijayo katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kesho jioni kikosi kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili katika Uwanja wa Mo Simba Arena ili kujiweka tayari kwa mechi ya marudiano.
Advertisement
Pamoja na kupoteza mchezo uliopita bado hatujapoteza malengo ya kufuzu na kutinga nusu fainali ya michuano hii.