Baada ya kuwasili Dar wachezaji watapewa ruhusa ya kwenda kukutana na familia zao na siku inayofuata kikosi kitarejea mazoezini.
Tukiwa nchini Sudan tumecheza mechi mbili za kimataifa dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana ambayo tuliifunga mabao 4-2 na wenyeji Al Hilal ambapo tulipoteza kwa bao moja.
Advertisement
Tunategemea kucheza mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Djibouti, Arta Solar 7 Jumamosi Septemba 3.