Simba Sports Club
News

Timu yaanza safari kuelekea Suez

1 Apr 2025

Baada ya kufika Suez kikosi kitafanya mazoezi kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Misri ambapo nyumbani itakuwa saa moja usiku katika Uwanja wa Suez Canal ambao utatumika kesho kwa mchezo.

Kikosi kimepata muda wa siku nne wa kufanya mazoezi nchini Misri ambapo wachezaji wamezoea mazingira na hali ya hewa ambayo ni baridi.

Advertisement

Wachezaji wote 22 tuliosafiri nao wapo kwenye hali nzuri na tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho ambao tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

Back to homepage
Share this story