Simba Sports Club
News

Timu yaanza mazoezi kujiandaa na Constantine

30 Nov 2024

Baada ya ushindi wa bao moja tuliopata dhidi ya Bravo FC kutoka Angola siku ya Jumatano wachezaji walipewa mapumziko mafupi kabla ya leo kurejea mazoezini kuendelea na maandalizi.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo yaliyofanyika katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena na kuongozwa na Kocha Mkuu Fadlu Davids na wasaidizi wake.

Advertisement

Kikosi chetu kinatarajiwa kuondoka nchini Jumatano ya Disemba 4 kikiwa na wachezaji 22 tayari kwa mtanange huo.

Mchezo wetu dhidi ya Constantine utapigwa katika Uwanja wa Chahid Hamlaoui saa 11 jioni nchini Algeria ambapo hapa nyumbani itakuwa saa moja usiku.

Back to homepage
Share this story