Baada ya mchezo wa jana tuliopata sare ya bao moja dhidi ya Namungo leo kikosi kimeanza mazoezi moja kwa moja kwa ajili ya mtanange huo muhimu dhidi ya Azam.
Mazoezi hayo yamefanyika katika Uwanja wa Majaliwa na wachezaji wote wameshiriki wakiwa katika hali nzuri.