Timu itaondoka na kikosi kamili tulichokisajili kwa msimu ujao wa ligi chini ya kocha Roberto Oliviera 'Robertinho' na benchi zima la ufundi.
Wachezaji wapya tuliowaasjili wa ndani na wale wa kimataifa nao watakuwa sehemu ya kambi hiyo nchini Uturuki.
Advertisement
Kambi ya Uturuki ni mapendekezo ya benchi la ufundi ambao wanaamini wachezaji watapata utulivu na kuyashika mafundisho watakayopewa.
Kikiwa nchini Uturuki tunategemea kikosi chetu kitapata mechi tatu za kirafiki kabla ya kurejea nchini mwishoni mwa mwezi huu.