Simba Sports Club
News

Timu kurudi Dar leo Asubuhi

26 Feb 2023

Kikosi kinarejea kikiwa na matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanikiwa kupata pointi tatu muhimu ugenini.

Baada ya kufika nyumbani wachezaji watapewa mapumziko ya siku moja kwenda nyumbani kukutana na familia zao na kupumzisha miili na akili kufuatia kazi ngumu waliyofanya.

Advertisement

Kikosi kitarejea mazoezini Jumatatu kujiandaa na mchezo wa hatua ya 16 bora wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya African Sports kutoka Tanga utakaopigwa Alhamisi saa moja usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Back to homepage
Share this story