Simba Sports Club
News

Timu kurejea nchini leo

7 Dec 2021

Kikosi chetu kinatarajia kurejea jijini Dar es Salaam leo kutoka Zambia ambapo moja kwa moja kitaingia kambini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Juzi Jumapili kikosi kilishuka katika Uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka kuikabili Red Arrows na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Advertisement

Jana timu ilifanya mazoezi ya gym asubuhi na jioni kilifanya uwanjani ili kuwaweka fiti na kurejesha utimamu wa mwili kwa wachezaji.

Maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Yanga yalianza nchini Zambia na yataendelea mara tu kikosi kitakapowasili.

Back to homepage
Share this story