Simba Sports Club
News

Timu kurejea mazoezini kesho kujiandaa na Namungo

13 Feb 2025

Mchezo dhidi ya Dodoma ulipangwa kufanyika Jumamosi, Februari 15 lakini wenzetu walipata ajali hivyo Bodi ya Ligi ilitangaza jana kuwa mchezo huo umeahirishwa.

Mechi yetu inayofuata itakuwa dhidi ya Namungo FC ambayo itapigwa katika Uwanja wa Majaliwa, Februari 19 siku ya Jumatano saa 12:30 jioni.

Advertisement

Wachezaji wote watarejea kesho na moja kwa moja wataanza maandalizi ya mchezo huo ambao malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda.

Back to homepage
Share this story