Baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC uliopigwa Jumapili iliyopita wachezaji walipewa mapumziko ambapo sasa watatakiwa kurejea mazoezini Disemba 29.
Wachezaji ambao watarejea mazoezini ni wale ambao hawapo kwenye majukumu ya timu za Taifa zinazoshiriki michuano ya AFCON itakayofanyika nchini Morocco kuanzia Disemba 21.
Advertisement
Wachezaji ambao watashiriki michuano ya AFCON ni Yakoub Suleiman, Shomari Kapombe, Wilson Nangu, Yusuph Kagoma, Kibu Denis na Morice Abraham ambao wapo katika kikosi cha Tanzania 'Taifa Stars'.
Nyota mwingine ambaye atashiriki michuano ya AFCON ni mshambuliaji Steven Mukwala akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes'.