Simba Sports Club
News

Timu kupaa mchana kuifuata Mbeya City

15 Jan 2022

Kikosi cha wachezaji 26 kitasafiri kuelekea jijini Mbeya leo saa nane mchana tayari kwa mchezo wetu wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Jumatatu Uwanja wa Sokoine.

Baada ya kurudi kutoka Visiwani Zanzibar jana, wachezaji walipewa mapumziko ya kwenda kuonana na familia zao na leo wamerejea tayari yakwa safari.

Advertisement

Mchezo dhidi ya City tumeupa umuhimu wa kipekee kwani tunahitaji alama tatu ndiyo maana tumeondoka na kikosi kizima.

Baada ya kuwasili Mbeya leo kikosi kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili (recovery) na kesho mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wenyewe Jumatatu.

Back to homepage
Share this story