Simba Sports Club
News

Timu kuondoka usiku kuifuata Ihefu

8 Apr 2023

Kikosi kitaondoka na wachezaji 22 benchi la ufundi pamoja na Viongozi kutoka kwenye Menejimenti kamili kwa mchezo huo.

Ingawa tumetoka kuwafunga mabao 5-1 kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup jana lakini hatutawadharau Jumatatu hivyo tumejipanga vizuri kuwakabili.

Advertisement

Wakati ligi ikiwa inaelekea ukingoni kila mchezo tunaupa umuhimu mkubwa na lengo ni kuhakikisha tunapata pointi tatu katika kila mechi

Mchezo wetu dhidi ya Ihefu utapigwa Jumatatu saa 10 jioni katika Uwanja wa Southern Highland, Mbarali Mbeya.

Back to homepage
Share this story