Kikosi kitasafiri kupitia nchini Uturuki kabla ya kutua Morocco tayari kwa kambi hiyo itakayovhukua siku tano.
Uongozi umeamua kupeleka timu Morocco mapema kwa lengo la kuwafanya wachezaji kupata muda wa kutosha wa kupumzika pamoja kuzoea hali ya hewa ili siku ya mchezo wasipate changamoto yoyote ya kimazingira.
Advertisement
Taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa inaeleza kuwa kwa sasa Morocco kuna baridi kali hivyo tumeamua kwenda mapema kwa lengo la kuzoea mazingira.
Timu itafikia Casablanca na kuweka kambi kabla ya kwenda mjini Barkane kuwakabili wapinzani wetu RS Barkane.