Kabla ya kuondoka kikosi kimefanya mazoezi asubuhi katika uwanja wetu wa Mo Simba Arena kwa ajili ya kuwaweka sawa wachezaji.
Morali ya wachezaji ipo juu na lengo letu la kwanza ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho kama ilivyo katika malengo yetu tuliyojiwekea.
Advertisement
Tumeshinda mechi zetu tatu za mwisho za nyumbani sasa tumejipanga kuhakikisha michezo miwili ya Nyanda za Juu Kusini iliyobaki kukamilisha msimu tunashinda ili kuendelea kuwapa furaha mashabiki wetu.