Kikosi kitapitia Doha Qatar na kuunganisha ndege mpaka Casablanca na baadae kuunganisha tena hadi Marrakech.
Timu inatarajia kufika Marrakhech kesho mchana na wachezaji watapata saa chache za kupumzika na jioni watafanya mazoezi ya utimamu wa mwili.
Advertisement
Kuanzia Alhamisi kikosi kitaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuivutia kasi Wydad katika mchezo ambao tunaamini utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya.