Kikosi kinatarajia kufika Lindi usiku ambapo wachezaji watapata mapumziko na kesho watafanya mazoezi ya mwisho kujiweka sawa kabla ya kushuka dimbani Jumatano.
Baada ya mchezo wa Jumatano kikosi kitabaki huko huko Lindi kujiandiaa na mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Azam FC utakaopigwa mwishoni mwa wiki.