Simba Sports Club
News

Timu kuondoka mchana kuelekea Mtwara

5 May 2023 By simbasc 157 views
Kikosi chetu kitaondoka muda mfupi ujao kutoka hapa Ruangwa kuelekea Mtwara tayari kwa mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Azam FC utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Kabla ya kuondoka Ruangwa kikosi kimefanya mazoezi asubuhi katika Uwanja wa Majaliwa ili kuwaweka sawa wachezaji. Wachezaji wote waliopo kikosini wapo kwenye hali nzuri tayari kupambania timu kufanya vizuri ili tutinge fainali ya michuano hiyo. Morali za wachezaji zipo juu kuanzia uwanja wa mazoezi, wanapokuwa wamepumzika au wakati wa kula wanazungumza kuelekea mchezo huo. Mchezo wetu dhidi ya Azam utapigwa Nangwanda Jumapili kuanzia saa 9:30 Alasiri.
Advertisement
Back to homepage
Share this story