Simba Sports Club
News

Timu kuondoka kesho saa tatu usiku

12 May 2025

Awali kikosi kilikuwa kimepanga kuondoka kesho saa 11 alfajiri lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu muda umesogezwa mbele na kitaondoka saa tatu usiku.

Kikosi kitaondoka na Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na kitafika katika Jiji la Casablanca ambapo kitaweka kambi ya siku mbili.

Advertisement

Baada ya kambi hiyo kitasafiri hadi katika mji wa Oujda ambapo ndipo kutapigwa mchezo huo wa fainali.

Back to homepage
Share this story