Simba Sports Club
News

Timu kuondoka kesho kuifuata TRA Arusha

6 Apr 2026

Baada ya kufika Arusha kesho jioni kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili na Jumatano kitafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kushuka dimbani Alhamisi.

Baada ya mchezo huo kikosi kitabaki jijini Arusha kwa ajili ya mechi ya hatua ya 16 bora ya CRDB Federation Cup dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Sheikh Amri Abeid Aprili 12.

Advertisement

Tutacheza mechi ya mwisho jijini Arusha, Aprili 15 dhidi ya Fountain Gate ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya NBC pia katika dimba hilo hilo la Sheikh Amri Abeid baada ya hapo timu itarudi Dar es Salaam.

Kesho kikosi kitaondoka na wachezaji wote kutokana na mechi hizo tatu ambazo zote tumezipa umuhimu sawa.

Back to homepage
Share this story