Simba Sports Club
News

Timu Kuondoka Kesho jioni kuifuata Vipers

22 Feb 2023

Kabla ya kuondoka kikosi kitafanya mazoezi asubuhi katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena ili kuwaweka sawa wachezaji.

Tumeamua kuondoka na kikosi kamili kwa kuwa tunaenda Uganda tukiwa na lengo la kuhitaji ushindi.

Advertisement

Ushindi katika mchezo dhidi ya Vipers utarejesha matumaini yetu ya kuvuka hatua hii ya makundi ndiyo maana tumechukua tahadhari zote.

Mchezo dhidi ya Vipers utapigwa katika Uwanja wa St. Mary's wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15,000 Jumamosi Februari 25, saa moja usiku.

Back to homepage
Share this story