Simba Sports Club
News

Timu kuondoka kesho asubuhi kuelekea Tabora

27 Oct 2025

Kikosi kitaondoka kwa usafiri wa Ndege kikiwa na wachezaji 22 benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi.

Kesho jioni kikosi kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili na keshokutwa kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Advertisement

Timu itasafiri ikiwa na lengo moja la kupambana mwanzo mpaka mwisho ili kuhakikisha alama tatu ugenini zinapatikana.

Mchezo dhidi ya TRA utakuwa ni wa kwanza wa ugenini kufuatia mechi mbili za mwanzo tulizocheza dhidi ya Fountain Gate FC na Namungo kucheza nyumbani.

Back to homepage
Share this story