Simba Sports Club
News

Timu kuondoka kesho alfajiri kuelekea Tunisia

20 Jan 2026

Kikosi kitaondoka na wachezaji 22 ambapo kitapitia Instanbul nchini Uturuki kabla ya kuunganisha Ndege mpaka Tunisia.

Tunatarajia kikosi kupata siku mbili za kufanya mazoezi na wachezaji kuendelea kuzoea mazingira ya Tunisia.

Advertisement

Pamoja na ugumu ambao tunategemea kukutana nao lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya kwenye mchezo huo.

Mchezo wetu dhidi ya ES Tunis utapigwa katika Uwanja wa Olympique De Rades, Jumamosi saa moja usiku kwa saa za Tanzania.

Back to homepage
Share this story