Timu itaondoka na wachezaji 22 tayari kwa mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wetu.
Kabla ya kuondoka leo asubuhi kikosi kimefanya mazoezi katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena kuwaweka sawa wachezaji kabla ya kuanza safari.
Advertisement
Kikosi kilianza mazoezi wiki moja iliyopita na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri morali ipo juu kuhakikisha tunashinda na kupata alama tatu muhimu ugenini.
Tutashuka katika mchezo huo tukijua utakuwa mgumu na tunawaheshimu Singida lakini tupo tayari kuhakikisha tunashinda.