Mchezo huo utafanyika Benin badala ya Ivory Coast ambapo ni nyumbani kwa ASEC kutokana na viwanja vyao kuwa kwenye ukarabati mkubwa ikijiandaa na michuano ijayo ya AFCON.
Kikosi kitaondoka saa tisa alfajiri na Ethiopia Airline kikiwa na wachezaji 24, benchi la ufundi na viongozi.
Advertisement
Tutaingia katika mchezo huo tukiwa na lengo la kutafuta alama tatu muhimu ili kujihakikishia nafasi ya kuingia robo fainali ya michuano hiyo.