Simba Sports Club
News

Timu kuondoka Ijumaa kuifuata ASEC Benin

17 Mar 2022 By simbasc 981 views

Kikosi chetu kitaondoka Ijumaa alfajiri kuelekea nchini Benin kwa ajili ya mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Jumapili saa moja jioni.

Mchezo huo utafanyika Benin badala ya Ivory Coast ambapo ni nyumbani kwa ASEC kutokana na viwanja vyao kuwa kwenye ukarabati mkubwa ikijiandaa na michuano ijayo ya AFCON.

Advertisement

Kikosi kitaondoka saa tisa alfajiri na Ethiopia Airline kikiwa na wachezaji 24, benchi la ufundi na viongozi.

Tutaingia katika mchezo huo tukiwa na lengo la kutafuta alama tatu muhimu ili kujihakikishia nafasi ya kuingia robo fainali ya michuano hiyo.

Back to homepage
Share this story