Kikosi kitashuka dimbani Jumanne katika Uwanja wa Ilulu kuikabili miamba hiyo ya Kusini katika mchezo ambao tunategemea utakuwa na ushindani wa kutosha.
Kwa sasa kila mchezo uliopo mbele yetu tumeupa umuhimu mkubwa kama fainali ili kuhakikisha tunamaliza vizuri msimu wa ligi.