Simba Sports Club
News

Timu kuondoka Alfajiri kuifuata Mashujaa

30 Oct 2024

Kikosi kinaondoka na wachezaji 22 na benchi zima la ufundi linaloongozwa na kocha, Fadlu Davids kwa ajili ya mchezo huo ambao utapigwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika Ijumaa saa 10 jioni.

Baada ya kikosi kufika Kigoma kesho jioni kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Lake Tanganyika kujiweka sawa kabla ya mtanange wenyewe.

Advertisement

Tutaingia kwenye mchezo wa Ijumaa tukiwa na kumbukumbu ya mshindi mnono wa mabao 3-0 tuliopata katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo FC.

Mara ya mwisho kucheza mechi ya Ligi dhidi ya Mashujaa katika Uwanja wa Lake Tanganyika ilikuwa Februari 3 mwaka huu na tuliibuka na ushindi wa bao moja lililofungwa na Said Ntibazonkiza kwa mkwaju wa penati.

Back to homepage
Share this story