Simba Sports Club
News

Timu kuondoka alfajiri kuifuata ASEC Ivory Coast

19 Feb 2024

Kikosi kitaondoka na jumla ya wachezaji 23 benchi zima la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi kutoka kwenye Menejimenti.

Lengo la kuondoka mapema ni kutokana na umbali wa safari na tunahitaji wachezaji wetu wapate muda wa kuzoea mazingira kabla ya siku ya mchezo.

Advertisement

Mchezo dhidi ya ASEC ni muhimu kwetu kupata ushindi ili tujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali ndio maana tumechukua tahadhari zote.

Mchezo wetu dhidi ya ASEC utapigwa katika Uwanja wa Felix - Houphouet - Boigny saa moja usiku kwa saa za Ivory Coast ambapo Tanzania itakuwa saa nne usiku.

Back to homepage
Share this story