Simba Sports Club
News

Timu kuondoka alfajiri kuelekea Misri

29 Jul 2025

Timu itakwenda kuweka kambi katika mji wa Ismailia kama ilivyokuwa msimu uliopita tukiwa na wachezaji wote ambao tunategemea kuwatumia katika msimu huu.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema wachezaji pekee ambao hawataambatana na timu ni wale waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa inayojuandaa na michuano ya CHAN.

Advertisement

"Kikosi chetu kitaondoka kesho alfajiri kuelekea Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu tukiwa na nyota wetu wote isipokuwa waliopo kwenye majukumu ya timu ya Taifa."

"Kikosi kitarejea nchini Agosti 28 tayari kwa kuanza msimu mpya wa mashindano 2025/2026 tukiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story