Kikosi chetu kitaingia kambini baada ya mazoezi ya leo jioni kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Mkwakwani Alhamisi saa 10 jioni.
Baada ya mchezo wa jana dhidi ya US Gandarmerie wachezaji walipewa nafasi ya kwenda kukutana na familia zao na jioni wataingia kambini kujiandaa na mchezo huo.
Advertisement
Tumefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na sasa tunarejesha nguvu kwenye ligi lengo likiwa ni lile lile kutetea taji letu.
Baada ya mchezo na Coastal kikosi kitasafiri kwenda Kilimanjaro kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Aprili 10.