Simba Sports Club
News

Timu kuifuata Kagera leo mchana

16 Dec 2021

Kikosi chetu kitaondoka mchana kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wetu ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Kaitaba Jumamosi, Desemba 18 saa 10 jioni ambapo tumejipanga kupata alama tatu muhimu.

Advertisement

Baada ya mchezo wa juzi wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya JKT Tanzania wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja kabla ya kuanza safari kuelekea Kagera.

Kikosi kizima kitasafiri ili kulipa nafasi benchi la ufundi kuchagua nani aanze lengo likiwa ni kupambana kuhakikisha tunarudi na alama zote tatu jijini Dar es Salaam.

Back to homepage
Share this story