Simba Sports Club
News

Timu kuifuata Green Buffaloes jijini Marrakech kesho

3 Nov 2022

Mechi zetu mbili za mwanzo dhidi ya ASFAR FC na Determine Girls zimefanyika hapa katika mji wa Rabat lakini huu wa mwisho utafanyika Marrakech.

Mchezo wetu dhidi ya Green Buffaloes utapigwa Jumamosi Novemba 5, saa nne usiku kwa saa za nyumbani Tanzania.

Advertisement

Safari ya kutoka Rabat mpaka Marrakech inachukua saa tatu ambapo baada ya kufika wachezaji watapumzika kabla ya kufanya mazoezi ya mwisho.

Tunahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya kutinga nusu fainali ambayo ni moja ya malengo tuliyojiwekea.

Back to homepage
Share this story