Kambi hiyo ni mualiko kutoka kwa Rais wa heshima wa klabu yetu Mohammed Dewji (Mo) ili kuipa nafasi timu ya kufanya maandalizi ya kujiandaa na michuano ligi ya Mabingwa Afrika.
Tukiwa Dubai tunatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki ambapo ratiba kamili itajulishwa baadaye.
Kikosi kitarejea nchini Januari, 14 tayari kwa mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Januari 17 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Akizungumzia kambi hiyo Robertinho amesema ni maamuzi sahihi ambayo yatampa nafasi ya kuangalia kikosi chake kwa mapana na kuanza kupandikiza falsafa zake akishirikiana na makocha wenzake Juma Mgunda na Selemani Matola.
"Ni uamuzi mzuri kwa Uongozi kunipa muda wa kufanya mazoezi na kikosi kwa utulivu ili kuniwezesha kuwajua wachezaji nakuwapa mbinu zangu," amesema Robertinho.