Mchezo huo utapigwa Februari 18 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo lengo letu ni moja kuhakikisha tunashinda nyumbani.
Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Horoya tuliopoteza kwa bao moja leo jioni kikosi itafanya mazoezi ya utimamu wa mwili kabla ya kesho kuanza safari ya kurudi nyumbani.
Advertisement
Kikosi kitapitia Ethiopia na kumpumzika kwa muda kabla ya kuendelea na safari ambapo tunatarajia kufika Dar es Salaam saa 9 alfajiri siku ya Jumanne.
Kikosi kikifika Dar wachezaji wataingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Raja.