Simba Sports Club
News

Timu imefanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na ASEC

12 Feb 2022

Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na morali ipo juu na kila mmoja amejitahidi kufanya vizuri ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi kesho.

Katika mchezo wa kesho tunahitaji kushinda katika uwanja wa nyumbani ili kujiweka kwenye mazingira mazuri katika mechi inayofuata.

Advertisement

Mchezo huo utaanza saa 10 jioni ambapo uongozi umesisitiza mashabiki kuendelea kununua tiketi mapema ili kuepusha usumbufu kesho.

Back to homepage
Share this story