Simba Sports Club
News

Tiketi za Simba Day zimeisha zote

31 Jul 2024

Hii ni rekodi nyingine tunaiweka kujaza uwanja kuelekea Simba Day siku nne kabla ya tukio lenyewe.

Tiketi za Platinum ziliisha siku ya kwanza baada ya kutangazwa zikifuatiwa na VIP A kabla ya leo majukwaa mengine yote kujaa.

Zoezi la kuuza tiketi lilianza wiki moja iliyopita lakini mwamko wa Wanasimba umekuwa mkubwa na leo tumeweka rekodi nyingine.

Viingilio vilikuwa kama ifuatavyo:

Mzunguko Sh. 5000

Advertisement

Machungwa Sh. 10,000

VIP C Sh. 20,000

VIP B Sh. 30,000

VIP A Sh. 40,000

Platinum Sh. 200,000

Back to homepage
Share this story