Taddeo ambaye alikuwa majeruhi ambapo alikosa baadhi ya mechi za karibuni amepona na amerejea mazoezini pamoja na wachezaji wenzake.
Taddeo amesema kwa sasa yupo fiti kushuka dimbani na analiachia benchi la ufundi kuamua kama watampanga katika mchezo wa Pamba Jumamosi.
Advertisement
"Mimi afya yangu inaendelea vizuri na niko fiti kwa sasa, kama mwalimu ataona inafaa anaweza kunipanga Jumamosi.
"Kikubwa nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani Jumamosi ili kutupa sapoti na tunaamini tutafanya vizuri," amesema Taddeo.