Dokta Kagabo amewataja wachezaji hao kuwa ni Clatous Chama, Luis Miqussone, Kibu Denis na mlinda mlango Aishi Manula.
Dokta Kagabo amefafanua hali za wachezaji wote zilizovyo mpaka sasa:
1. Chama na Luis bado wanauguza nyama za paja (harmstring) siku ya 10 leo, wanaendelea na tiba vizuri. Kuna uwezekano mkubwa wakajiunga na timu katika michezo mitatu au minne ya mwisho.
Advertisement
2. Kibu yupo Hatua za mwisho za matibabu ya enka leo ni siku ya nane anakaribia kuanza mazoezi mepesi siku chache zijazo.
3. Manula bado anauguza jeraha la nyama za paja kwenye Nyonga wiki 5 sasa, nae yuko hatua za mwisho kupona.