Simba Sports Club
News

Taarifa ya Daktari kuhusu Kagoma na Hamza

30 Oct 2024

Wawili hao hawajaonekana uwanjani kwa siku 10 sasa kutokana na majeraha hayo Dk. Kagabo ameweka wazi kuwa wanaendelea na matibabu.

Dk. Kagabo amesema Kagoma amepata changamoto ya nyonga wakati wa mechi dhidi ya Yanga ameshaanza matibabu na yupo kwenye hatua za awali ambapo ataendelea kupata tiba kwa wiki tatu hadi nne.

Advertisement

Dk. Kagabo ameongeza kuwa Hamza alipata changamoto ya nyama za paja wakati wa mechi dhidi ya Yanga na anaendelea na matibabu ambayo yapo kwenye hatua za mwisho.

"Wachezaji wetu wawili Kagoma na Hamza walipata majeraha katika mchezo dhidi ya Yanga na wanaendelea na matibabu na hivi karibuni wataanza mazoezi ya utimamu wa mwili," amesema Dk. Kagabo.

Back to homepage
Share this story