Simba Sports Club
News

TAARIFA KWA UMMA

6 Sep 2022

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mikataba ya Kocha wa viungo Sbai Karim na Kocha wa makipa Mohammed Rachid.

Uongozi wa klabu ya Simba unawashukuru Makocha hao kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila heri katika majukumu yao mapya.

Kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya KMC kikosi chetu kitakua chini ya Kocha msaidizi Selemani Matola.

Tayari mchakato wa haraka wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Simba Nguvu Moja.

Advertisement

Barbara Gonzalez

Afisa Mtendaji Mkuu

Simba Sports Club

06 Sept, 2022

Back to homepage
Share this story