Simba Sports Club
News

TAARIFA KWA UMMA

14 Jan 2025

Uamuzi huo wa CAF umeifungia klabu yetu mechi mbili, hata hivyo adhabu hiyo imepunguzwa kuwa mechi moja kucheza bila mashabiki pamoja na faini ya Dola elfu 40,000.

Hivyo tunapenda kuufahamisha umma kuwa tunaendelea kufanya taratibu ili kushughulikia uamuzi huo.

Advertisement

Kwa maamuzi hayo klabu inasitisha mauzo ya tiketi ya mchezo wetu dhidi ya CS Constantine na kwa mashabiki ambao wameshanunua tiketi tunaomba tiketi hizo zitatumika kwenye mchezo ujao wa robo fainali.

Klabu ya Simba itaendelea kusimamia taratibu, kanuni na sheria zinazozingatia usalama wa jumla katika michezo.

Back to homepage
Share this story